Mawaziri wa afya kutoka nchi 11 za Afrika magharibi wamekubaliana mpango wa kupambanan na ugonjwa wa Ebola katika ukanda wao.
Katika mkutano wa dharula nchini Ghana, mawaziri wameahidi kushirikiana kupambana na ugonjwa huu unaoelezwa kuwa hatari hivi sasa.Watu 759 wameathirika na Virusi vya ugonjwa huo nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone na watu 467 wamepoteza maisha.
Mkutano huo wa siku mbili uliandaliwa na Shirika la afya duniani,WHO.
Chini ya mkakati huo mpya, WHO itafungua kituo nchini Guinea kwa ajili ya kuratibu kiufundi utekelezwaji wa mikakati hiyo.
Mwandishi wa BBC kutoka Afrika magharibi Thomas Fessy amesema kutoa elimu juu ya ugonjwa huu ni muhimu zaidi kuliko kufunga mipaka ya nchi kupambana na ugonjwa
halikadhalika tamaduni na imani za kijadi katika baadhi ya maeneo vimesababisha ugonjwa wa Ebola kusambaa kwa kasi.
makundi mbalimbali yamekuwa yakiwavamia wafanyakazi wa afya na kuwashinikiza kufunga vituo vyao.
WHO tayari imepeleka wataalam zaidi ya 150 Afrika magharibi miezi michache iliyopita ili kupambana na Ebola.
Ugonjwa wa Ebola husambaa umeelezwa kutokuwa na kinga wala tiba, na unaua mpaka 90% ya walioathirika.
@peacethepresident
0 comments:
Post a Comment