Thursday, July 3, 2014
On 2:04 PM by Unknown in SPORTS No comments
BONDIA Floyd Mayweather Jr ameweka wazi mpambano wake wa marudia
no na
Marcos Rene Maidana mpambono huo ambao ameuweka wazi utapikwa september 13 MGM Grand, Las Vegas, Nevada kugombania mikanda ya ubingwa wa WBC welterweight title
WBA Super World welterweight title
Mayweather ambaye anatumainiwa akiwa ulingoni na pia ndio bondia ambaye anachukuwa mkwanja mwingi ukulinganisha na mabondia wengine duniani
Kiatu cha Nike Hypervenom cha mwaka 2014 kinavaliwa na wachezaji kama Welbeck, Neymar na Rooney kwenye kombe la dunia la 2014. Kiatu hichi cha Nike Hypervenom 2014 ambacho ni Hyper Punch Boot kilizinduliwamwezi wa Nne pamoja na kiatu kingine cha Nike cha kombe la dunia.
Hypervenom 2014 kinafana kwenye mchanganyiko wa rangi na Nike Mercurial Vapor X. Muundo wa Nike Hypervenom 2014 umeboreshwa kuwa na control zaidi.
Thursday, June 26, 2014
On 9:28 AM by Unknown in SPORTS No comments
Suareza alisema awali kuwa baadhi ya matukio yanayotokea uwanjani hayapaswi kugeuzwa kashfa
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uruguay Luis Suarez amefungiwa mechi tisa na shirikisho la kandanda duniani Fifa baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ta mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kwenye mechi yao ya kombe la dunia nchni Brazil.
Suarez pia amefungiwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya kandanda kwa miezi minne na kutozwa faini ya dola elfu mia moja.
Kutokana na adhabu hiyo Suarez sasa hatashiriki tena kwenye mechi zilizosalia za kombe la dunia.
Kutokana na adhabu hiyo iliyochukuliwa na kamati ya nidhamu ya Fifa Suarez sasa hatashiriki kwenye mechi ya raundi ya pili kati ya Uruguay na Columbia Juni tarehe 28.
Adhabu hiyo pia inamaanisha Suarez hatashiriki kwenye mechi za Uruguay zijazo za kombe la dunia endapo timu itazidi kusonga mbele na zile zijazo za kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.
Kamati hiyo ya nidhamu ya Fifa imesema Suarez hatakiwi kuingia kwenye uwanja wowote Uruguay inapocheza wakati wa adhabu hiyo ya kutocheza mechi tisa za kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya Fifa Claudio Sulser amesema:"Hatuwezi kuruhusu tabia duni kama hii uwanjani hasa wakati wa kombe la dunia kwani mamillioni ya mashabiki kote duniani wanafuatilia mashindano haya. Kamati ya Fifa imetilia maanani kila kitu kwenye kitendo hicho kabla ya uamuzi huo.Tayari tumemjulisha mchezaji huyo na shirikisho la kandanda la Uruguay.''
Mashabiki wengi duniani wamemshutumu vikali Suarez kwa kumng'ata mchezaji huyo wa Italia kwani hii ni mara ya tatu anapatikana na hatia hiyo.
Lakini mashabiki, waandishi wa habari wa Uruguay na shirikisho la kandanda nchini humo wamemtetea mchezaji wao,wakisema hizo ni njama za kumuangamiza Suarez ambaye huichezea Liverpool ya England
Wednesday, June 25, 2014
Justin Bieber amepata ajali ya gari akiwa katika gari lake la Cadillac Escalade wakati akiwakimbia mapaparazzi, Beverly Hills.
Kwa mujibu wa TMZ, Bieber alikuwa amekaa kwenye seat ya abiria ambapo gari lingine aina ya BMW liligonga mlango wa upande huo.
Kwa bahati nzuri, hakuna aliyeumia katika ajali hiyo na Justin alihamia kwenye gari nyingine na kuendelea na safari.
On 1:32 AM by Unknown in SPORTS No comments
FIFA wameanza kumchukulia hatua mshambuliaji wa Uruguay, Luis Suarez hatua baada ya kutuhumiwa kumng’ata mchezaji wa Italia, Giorgio Chiellinni.
FIFA imetoa tamko Jana jioni kuwa kufikia leo majira ya saa kumi jioni (muda wa Brazil) mchezaji huyo na shirikisho la mpira wa miguu la Uruguay kupeleka vielelezo kuthibisha utetezi wao juu ya tukio hilo.
Suarez alipoulizwa kuhusu tukio hilo alijitetea na kudai kuwa ilitokea wakati wanagombea mpira na kwamba alijigonga na sio kumng’ata.
“The only thing I know is that those are occurrences that happen on the pitch.” Aliwaambia waandishi wa habari.
Picha za television zinamuonesha Suarez akipeleka kichwa chake kwa Chiellinni na walipoanguka pamoja, mchezaji huyo wa Italia alionesha ishara kuwa ameng’atwa begani. Baadae alionesha bega lililoshambuliwa.
Chiellinni amehimiza hatua zichukuliwe dhidi ya Suarez.
Mchezaji huyo wa Uruguay ameshakutana na kesi za matukio ya kung’ata watu mara kadhaa.
Katika mechi hiyo Uruguay ilishinda 1-0 na imeingia katika hatua za mtoano.
Tuesday, June 24, 2014
On 10:58 PM by Unknown in SPORTS No comments
Suarez anashtumiwa kwa kumngata mlinzi wa Italia
Mshambulizi wa Uruguay Luis Suarez amekumbwa na kashfa mpya baada ya kuonekana kumngata Giorgio Chiellini wa Italia.
Suarez alionekana akiminya bega la Chiellini muda mchache kabla ya Diego Godin kufunga bao la ushindi la Uruguay dhidi ya Italia.
Chiellini aliangushwa chini na uchungu wa meno ya Suarez na alionekana akimkimbilia refarii akimvulia shati ilikuonesha alama ya meno begani lakini refarii akapuzilia mbali .
Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.
Suarez anatumumiwa kwa kumngata Chielleini
Suarez alionekana akigaaga uwanjani baada ya tukio hilo.
Japo refarii Marco Rodriguez hakuona tukio hilo la kutamausha Chiellini amesikika akisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuwa refarii huyo alipuzilia mbali maombi yake ya kutaka hatua ichukuliwe dhidi ya mshambulizi huyo ambaye aliadhibiwa kwa tukio lengine kama hilo akiichezea Liverpool misimu miwili iliyopita nchini Uingereza.
Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumngata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013
Suarez na refarii wa mechi hiyo Marco Rodriguez
Awali Suarez aliadhibiwa na shirikisho la soka la Uholanzi lilimuadhibu Suarez kwa marufuku ya mechi saba baada ya kumngata mchezaji wa PSV Eindhoven Otman Bakka wakati huo akiwa nahodha wa Ajax Amsterdam.
Mwaka wa 2010 Suarez aliunawa mkwaju ambao ulikuwa unaingia wavuni na kuinyima Ghana nafasi ya kuingia kwenye nusu fainali ya kombe la dunia .
On 2:09 PM by Unknown in SPORTS No comments
KIUNGO Ander Herrera anakaribia kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya wa Manchester United ya England, Louis van Gaal kwa dau la Pauni Milioni 28.4.
Mchezaji huyo wa Athletico Bilbao amekuwa akitakiwa na klabu hiyo ya Ligi Kuu England tangu msimu uliopita, lakini sasa kocha mpya wa Mashetani hao Wekundu, Van Gaal has anaelekea kufanya kweli kumnasa nyota huyo.
Anakuja: Ander Herrera anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Louis van Gaal Manchester United kwa Pauni Milioni 28.4
On 2:01 PM by Unknown in SPORTS No comments
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis Suarez alimng’ata Giorgio Chiellini.
Godin alifunga bao hilo dakika ya 81 na kipa Buffon wa Italia alilazimika kuingia uwanjani dakika ya mwisho kusaidia nguvu ya kusaka bao, Azzuri ikihtaji sare tu kusonga mbele.
Italia ilimpoteza mchezaji wake Marchisio aliyetolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Arevalo Rios dakika ya 60.
Mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo (kushoto) akibadilishana jezi na Edisnon Cavani wa Uruguay baada ya mechi
Rapper Bow wow ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha 106Park cha amebadili jina lake rasmi na sasa anataka aitwe jina lake halisi Shad Moss
Bow Wow ameandika kwenye video aliyoweka Instagram sababu za kubadili jina lake kuwa ni kuanza ukurasa mpya wa maisha na Bow Wow anao ni jina ambalo haliendani nae kwa hivi sasa.
“Baada ya BET awards sitatumia jina la Bow Wow tena. Nitatumia jina langu halisi Shad Moss. Tumefanya historia ndefu kama Bow Wo. Na sasa ni muda wa kuanza ukurasa mpya na challenge.”
Bow Wow anaona kama jina hilo ni la kitoto na sasa amekuwa anataka ajulikane kiofisi zaidi.
“Mimi ni baba, mfanyabiashara, mtangazaji wa TV, muigizaji na rapper. Ni muda wa Mr Moss kutake over.”
Mwaka 2001 alibadili jina kutoka Lil Bow Wow na kuitwa Bow Wow na sasa ni zamu ya Mr Moss
Monday, June 23, 2014
On 11:52 PM by Unknown in SPORTS No comments
WENYEJI Brazil wamekamilisha mechi za kundi lake, A kwa ushindi wa mabao 4-1 usiku wa kuamkia leo dhidi ya Cameroon Uwanja wa Nacional.
Mshambuliaji tegemeo Neymar alifunga mabao mawili dakika za 17 na 34, wakati mabao mengine yalifungwa na Fred dakika ya 49 na Fernandinho dakika ya 84.
Bao pekee la Simba Wasiofungika wanaoaga michuano hiyo bila hata pointi moja baada ya awali kufungwa pia na Croatia na Mexico, lilifungwa na Matip dakika ya 26.
Croatia nato ilimaliza na ushindi wa 3-1 dhidi ya Mexico, mabao yake yakifungwa na Rafael Marquez, Andres Guardado na Javier Hernandez. Bao la kufutia machozi lka Mexico iliyompoteza mchezaji wake Ante Rebic aliyetolewa kwa kadi nyekundu mwishoni mwa mchezo, lilifungwa na Ivan Perisic. Brazil inamaliza na pointi saba sawa na Croatia, lakini inakaa kileleni kwa wastani mzuri zaidi wa mabao
Nyota: Neymar amefunga mabao mawili dhidi ya Cameroon
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
- ENTERTAINMENT
- MUSIC
- SPORTS
Category
- ENTERTAINMENT
- MUSIC
- SPORTS
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
5:55 PM PT -- Meek just posted his first pic after prison -- chilling in a living room and cracking jokes about a friend's broken foot...
-
Mansoor himid,aliyewahi kuwa mwakilishi na wakati flani waziri asiyekua na wizara maalum na pia ni shemeji wa rais karume, Akutwa na silaha...
-
Mr Blue aka Kabayser ameanzisha taasisi ya ‘Micharazo Foundation’ itakayoanza kupokea wasanii wapya na pia itakuwa sehemu ya kukuza vipaj...
-
Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhum...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
Kiatu cha Nike Hypervenom cha mwaka 2014 kinavaliwa na wachezaji kama Welbeck, Neymar na Rooney kwenye kombe la dunia la 2014. Kiatu hichi c...
-
Mark Wahlberg 's massive home in Beverly Park, CA is finally complete ... 30,000 square feet strong ... and it's t...
-
Amber Rose was a guest on the Breakfast Club last week , and she threw some shade towards Tyga and Kylie Jenner, alluding that the two wer...
-
Nicki Minaj didn't seem to have big problems with hilarious memes appearing on the internet following the release of her...
Labels
- ENTERTAINMENT
- MUSIC
- SPORTS




















