Wednesday, August 6, 2014
On 6:51 AM by Unknown No comments
Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gedfrey Nzowa alisema jana kuwa Masogange alianza kuhojiwa juzi usiku baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini.
Nzowa alisema baada ya kuhojiwa, Masogange aliruhusiwa na kwamba yupo huru, ameachiwa bila masharti yoyote.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani naye alithibitisha kuhojiwa kwa msanii huyo akisema: “Hapa kuna kikosi kazi, kila mmoja alimhoji kwa wakati wake lakini kwa upande wa polisi tulimpekua na kumhoji lakini tumemwachia.”
Kamanda Selemani alisema Masogange alianza kuhojiwa juzi saa mbili usiku hadi jana saa nne asubuhi.
Hata hivyo, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Masogange alikana akisema kwa kifupi na kukata simu: “Hilo unalosema siyo kweli na sipo tayari kuzungumzia hilo… Siwezi kuzungumza na chombo cha habari kwa sasa, shida yako nini?”
Masogange alitawala vyombo mbalimbali vya habari nchini katikati ya mwaka jana baada ya kukamatwa Afrika Kusini akiwa na nduguye Melisa Edward wakiwa na ‘mzigo’ wa dawa hizo zenye thamani zaidi ya Sh6.8 bilioni.
Wasichana hao walinaswa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Nzowa alisema jana kuwa katika mahojiano hayo walimuuliza kuhusiana na ushahidi alioutoa huko Afrika Kusini kuwa dawa hizo za kulevya alipewa na mtu kutoka JNIA.
“Ni kweli tulikuwa tunamuhoji Masogange ili atueleze mtu gani aliyempa crystal methamphetamine kama alivyodai kuwa amepewa na mtu wa hapa JNIA,” alisema Nzowa.
Katika mahojiano hayo, Nzowa alidai kuwa Masogange alidai kuwa alipewa dawa hizo na mtu ambaye hamfahamu kwa jina lakini anaikumbuka sura yake.
Alisema baadaye walikwenda eneo ambalo walipeana dawa hizo na mtu asiyemjua jina lake kwa ajili ya kuweza kumtambua kama alikuwapo eneo hilo.
“Pia tulimuhoji kutaka kujua alikwenda Afrika Kusini kufanya nini, kwa sababu ipi, alimfuata nani na alifikia wapi,” alisema Nzowa.
“Pia tulimuhoji kutaka kujua alikwenda Afrika Kusini kufanya nini, kwa sababu ipi, alimfuata nani na alifikia wapi,” alisema Nzowa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Arnold Schwarzenegger was born and raised in Austria. But The Expendables 3 star looked like a true American as he left Cafe Roma in Beverly...
-
baada ya BET kutoa fulsa kwa production companies nyingi kwa ajili ya kurusha reality show ya chris brown sasa cheki akivyo sema..
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis ...
-
Baada ya habari za ndege ya Malaysia airline hivi sasa ajali nyingine imetoka karibu kabisa na Tanzania ambapo ni nchini Uganda. Ndege hiy...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Karrueche Tran mrembo ambae ni mpenzi wa mwimbaji staa wa dunia Chris Brown alihusika kama mtangazaji na kuhoji watu mbalimbali wal...
0 comments:
Post a Comment