Thursday, July 3, 2014

On 1:20 PM by Unknown in ,    No comments
Davido’s BET victory has just been acknowledged by American rapper Meek Mill with whom he hung out in a club a short while before the awards in L.A. Meek Mill posted the Tweet below directed at Davido’s Instagram giving a shout out to him
Davido was also rocking the 24Karat gold Meek Mill headphones in a photo during the week.
On 12:37 PM by Unknown in , ,    No comments
Kiatu cha Nike Hypervenom cha mwaka 2014 kinavaliwa na wachezaji kama Welbeck, Neymar na Rooney kwenye kombe la dunia la 2014. Kiatu hichi cha Nike Hypervenom 2014 ambacho ni Hyper Punch Boot kilizinduliwamwezi wa Nne pamoja na kiatu kingine cha Nike cha kombe la dunia. Hypervenom 2014 kinafana kwenye mchanganyiko wa rangi na Nike Mercurial Vapor X. Muundo wa Nike Hypervenom 2014 umeboreshwa kuwa na control zaidi.
On 12:22 PM by Unknown in ,    No comments
Baada ya kuzushiwa kuwa ametofautiana na Rapper wa Kike Iggy Azalea, Rapper kutoka Young Money Nicki Minaj ameweka wazi kuwa hajawahikuwa na beef na msanii huyo na hana mpango a kuanzisha beef na Iggy ilikupata umaarufu zaidi. Nicki Minaj alipokea tuzo ya Msanii Bora wa Hiphop Wa Kike kwenye tuzo za Bet na alishangilia kwa kucheza kama alivyocheza Iggy kwenye video yake ya Fancy kitendo kilicho tafsiriwa kwana Diss kwa Iggy kutoka kwa Minaj. Ukiacha kitendo hicho pia inasemekana Nicki aliwahi kukashifu kitendo cha Iggy kuandikiwa mistari na mtu asiyetaka kutajwa. Waandishi hawa huitwa GhostWriters Nicki Minaj ametumia twitter kutoa maelezo kuwa amefuahishwa na mafanikio ya Iggy na anapenda kuona wasanii wakike wakifanya vizuri ata zaidi yake.
On 11:26 AM by Unknown in ,    No comments
Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL), ndani ya Stetion maarufu hapa Tz yaana nazungumzia CLOUDS Fm utaelewa nini ninachozungumzia mpaka sasa. Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu kama, DJ FETTY, ADAM MCHOVU na B12 waliziweka ndani ya studio za Clouds live huku wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya huko ndani ya studio. Sakata hilo limesababisha na kutoelewana baina ya hawa watangazaji juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji walikuwa nataka kujua nini zaidi kilitokea kupitia kipindi cha Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni nn? Baada ya massage nyingi sana kwenye kipindi cha hekaheka ilibidi wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta Adam, Fetty na B12 kujua nini kilichosababisha kuchapana makonde wakati bado kipindi kikiwa hewani. Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na kumpigia B12 ambaye alikataa kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la kutwangana huku akisema mambo yote yapo kwa uongozi.....
PICHA YA STUDIO ZA CLOUDS BAADA YA KUZICHAPA Simu ya pili ilimuendea ADAM MCHOMVU ambaye pia aligoma kuelezea kilichotokea jana, baada ya Muda mfupi Adam alimkabidhi Dem wake ili azungumze na mwandishi, huku akijua kwamba harikodiwi kumbe yupo hewani, alikiambia kipindi cha hekaheka kwamba ADAM amemaind na hataki kuongea na simu!! Simu ya tatu ilienda kwa DJ FETTY, Ambapo iliita bila majibu kwamba ilikuwa haipatikani.. Chanzo kinasema kwamba baada ya ugomvi, vifaa mbalimbali vya studio vimeharibiwa wakati wa ugomvi huo kama MIC, COMPUTER Meza nk. Endelea Kufuatilia Hapa ili ujua ni hatua Gani watachukuliwa watangazaji hawa kwa kukosa utovu wa Nidha CHANZO CHA HABARI Hot Hewz Daily.

Friday, June 27, 2014

On 2:29 PM by Unknown in ,    No comments
Barnaba anajitayarisha kufanya video ya wimbo wake mpya “Wahaladee” na tayari ametangaza kuwa video Queen wa kazi hiyo mpya atakuwa Mama Steven ambaye ni mpenzi na mama mtoto wa wa msanii Barnaba ” Sina la kuandika zaidi ya Asante wife kukubali kuwa Video Qwen Wangu kwenye #Wahaladee Ilove uu Verry moo much….. Sema nakulipa oky, sema sio nyingi, uwii sipati Picha apo Location … Uwiii, uwiii ,mama ndani ya shela baba ndani ya bangoooooo. “
On 10:20 AM by Unknown in    No comments

Thursday, June 26, 2014

On 8:41 AM by Unknown in ,    No comments
Mwanamuziki Diamond amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya wasanii kuwa aliwaibia idea au nyimbo zao na kuzifanya zake. Ameeleza kuwa malalamiko yao hayana ukweli kwa kuwa kuna maneno ya ambayo yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na watu wote lakini anapoyatumia hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na kudai kuwa ameiba idea yake.
Ametoa mfano wa nyimbo kama Moyo Wangu ambayo anasema baada ya kuimba wasanii wengine waliimba pia lakini hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa kwa sababu neno hilo linaweza kutumika na kila mtu kwa ufundi wake. Diamond ameeleza pia kuhusu tuhuma za Wababa (ingawa hakumtaja jina) kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na sasa anauita Mdogomdogo. “Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni nyimbo. “Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.” Kwa hisani: Timesfm.co.tz
On 8:36 AM by Unknown in ,    No comments
Mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa studio za Burn Records, Sheddy Clever ameamua kuuza vifaa vyote vya studio yake kwa mtu yeyote anaetaka kuvimiliki
Kupitia Instagram, Sheddy ameweka picha ya vifaa vyake anavyouza na kutoa namba ya simu kwa mawasiliano. “Habari ….. Vifaa vya s2dio @burnrecordz vyooote vinauzwa kwa anaehitaji cheki +255654067053 -> Mic, keyboard ,monitor speaker alesis,meza ya s2dio, mic stand, sound card, na vingine cheki hum.” Akiongea na sammisago.com Sheddy ameeleza kuwa ameamua kuuza vifaa hivyo ili anunue vifaa vipya kabisa na vya kisasa zaidi, na kwamba chanzo cha uamuzi huo ni fedha alizozipata kupitia wateja wengi zaidi aliowapata tangu alipotoa wimbo wa Diamond ‘My Number One’. Sheddy Clever aliutengeneza wimbo wa My Number One bila malipo lakini hivi sasa anakiri kupata mafanikio makubwa kupitia wimbo huo ambao umempa nafasi Diamond kushiriki kaika tuzo za MTV MAMA mwaka huu. Kama unahitaji kumiliki vifaa vilivyotumika kuandaa nyimbo kali za Sheddy, mpigie kupitia 0654067053.
On 8:26 AM by Unknown in ,    No comments
Beyonce aliandika kwenye website yake ujumbe maalum unaosimulia maisha yake kwa kukumbuka matukio yaliyokuwa yanamgusa MJ. Aliandika kuwa wakati anaanza muziki, producer wake wa kwanza alimtaka aangalie performance ya Michael Jackson ‘Who’s Loving You’ kwa masaa kadhaa. Alieleza kuwa alimwambia afanye hivyo kwa lengo la kujifunza kuwa unaweza hata kusikia roho yake wakati anaperform. “What he wanted me to learn was his soul. You could hear his soul. And he was this little kid who hadn’t experienced love but he was a vessel.For whatever reason he could evoke more emotion than an adult. It was so raw and so pure. It was these little things that he did that were just swag. It’s something that’s God given.” Aliandika Beyonce. Alieleza kuwa alijifunza kuwa sio lazima kila wakati utumie technique na kufuata hisia zako. “Michael Jackson alinibadilisha, na alinisaidia kuwa mwanamuziki kwa jinsi nilivyo, asante Michael.”

Wednesday, June 25, 2014

On 1:16 AM by Unknown in    No comments
Raper wa mziki wa bongo flavor heat maker wa full nga’ae ngae, nimewasamehe na nyingine nyingi ambae alifahamika zaidi alipokuwa akililiongoza kundi la Mexicana lacavela ambae kwa sasa ni msanii anaemilikiwa na rec lable ya vipaji tz kama solo artist rec lable ambayo mpaka sasa mmiliki wake hajataka kufahamika lakini inasemekana ni mtu mashuhuri na mkongwe kwenye tasnia ya mziki wa bongo flavor jana almanusura awekwe ndani kwa kudaiwa kuchukua hela za show na kutokwenda kwenye show hiyo Baghdad ameeleza ya kuwa ni siku chache zimepita akiwa anapigiwa simu na namba ngeni na kuambiwa vip kuhusu show ya vunja jungu mkoani lindi tar 29 na Baghdad kutoonyesha hali ya kujua jambo lolote na kadri promoter alipokuwa akimtishia Baghdad juu ya kuchukua kiasui cha fedha kama advance ya show Baghdad aliendelea kumjibu ovyo kwa kuwa hakupokea kiasi chochote cha fedha na hana taarifa yoyote. Erick mbudagazi ambae ni promoter wa onyesho hilo aliamua kutafuta mbinu yakumkamata Baghdad na kuamua kumtumia msichana ambae jina lake halikufahamika ili kumnasa Baghdad. Baghdad aelezea ilivyokuwa, nilikuwa natoka kuoga niliporudi nimkuta bby wangu akiwa amekwazika na sikujua tatizo lakini alikuwa na simu yangu na nilipoichukua aliniuliza ni nani huyo na nilipotazama kwenye whatsaap nilikuta picha za ajabu za msichana ambae anajifanya tulishawahi kukutana kwenye show Dodoma na tulitongozana sema alipoteza simu na kwa sasa yuko dar amefikia kempisk na atakaa kwa muda wa siku 3 na ataomba kampani yangu kama sintojali, nilikuwa na nia ya kumkatalia lakini baby wangu ili aridhike alisema nimkubalie na Yule mdada aliniambia tuonane mlimani sity anataka akafanye shoping na aninunulie simu mpya, nilitekeleza ili nisimkere mpenzi wangu. Nilianza safari na nilipoofika nilionana nae ghafla kabla ya kumaliza maongzi wajkatokea watu 3 aliovaa kiraia na wawili wamevaa nguo za ki polisi, promoter alionekana kuwa mpole baada ya kuniona na aliniuliza wewe ndie Baghdad nikamwambiea ndie mimi na akawa anazidi kussisitiza kuwa mimi ndie Baghdad feki maana Baghdad anaemjua yeye ni mnene. Maongezi yaliendelea jamaa akishinikiza nimrejeshee hela yake na n ilipojaribu kumuuliza njia aliyofanya malipo na alipopata namba yangu alisema alipowasiliana na Baghdad alimueleza yuko Kenya kwenye show hivyo alitumia namba ya airtel na alimpa namba ya 0652 89 48 71 ambapo alisema atarejea baada ya wiki moja na alimuelekeza kuna mtu ambae ndie manager wake kwa sasa yuko magomeni atamtafuta waingie nae mkataba na promoter anadai alionana na jamaa alieelekezwa na kumlipa na kusaini mkataba baada ya wiki kupita promoter alikuwa anahitaji picha ya msanii ili anprint posters ili zianze kwenda kubandikwa na alipopiga namba aliopewa na Baghdad alikuta habari tofauti na kutokuelewana. Baghdad amesema iluitumia muda kumuelewesha promoter lakini mwisho alielewa baada ya Baghdad kutokukutwa na hatia yoyote na baadae walikubaliana kukusanya nguvu ya kumtafuta kwa pamoja Aidha Baghdad ameomba samahani kwa mashabiki wake, na wadau kwa ujumla na kusema kukaa kwake kimya alikuwa akijipanga hivyo muda wowote ataachia kazi yake mpya alioifanya vipaji rec ikiwa ni mikonoya producer wake abah prossec aliomshirikisha dream nyota mpya anekuja kwa kasi kwenye mziki wa bongo flavor ifahamikayo kwa jina la haiters. Aidha Baghdad amesema ya kuwa kwa mtu yoyote anaehitaji kuwasiliana nae kwa lolote awasiliane nae kwa no 0652 89 48 71 kwa simu ya mkononi na whatssap Instagram bagh­_dad Twitter kwekapraygod Facebook Baghdad pg kweka. Mwisho alisema mungu ibariki vipaji tz, mungu ibariki bongo flavor mungu walaanio matapeli waliotapeli kwa kutenda, kwa kunena au kwa kufikiri

Tuesday, June 24, 2014

On 1:40 PM by Unknown in ,    No comments
Prince Dully Sykes ni msanii ambaye siku zote anapewa heshima ya kukaa kwenye game kwa muda mrefu bila kuchuja akiwa na hits kibao
Mwimbaji huyo ameomba msaada wako wewe shabiki wake kwa kumsaidia kupata model wa kike au wa kiume, au kama wewe unaweza kuwa na sifa hizo msaada ambao unaweza kugeuka kuwa deal kwa upande wako. “HABARI MARAFIKI ZANGU NAHITAJI MODELS KIKE/KIUME KWA AJILI YA VIDEO SO ATAKAE ONA ANAWEZA KUNISUPPORT ANICHEK KWA INSTAMSG.” Dully Sykes ameandika kwenye Instagram
On 1:33 PM by Unknown in , ,    No comments
Rapper Bow wow ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha 106Park cha amebadili jina lake rasmi na sasa anataka aitwe jina lake halisi Shad Moss
Bow Wow ameandika kwenye video aliyoweka Instagram sababu za kubadili jina lake kuwa ni kuanza ukurasa mpya wa maisha na Bow Wow anao ni jina ambalo haliendani nae kwa hivi sasa. “Baada ya BET awards sitatumia jina la Bow Wow tena. Nitatumia jina langu halisi Shad Moss. Tumefanya historia ndefu kama Bow Wo. Na sasa ni muda wa kuanza ukurasa mpya na challenge.” Bow Wow anaona kama jina hilo ni la kitoto na sasa amekuwa anataka ajulikane kiofisi zaidi. “Mimi ni baba, mfanyabiashara, mtangazaji wa TV, muigizaji na rapper. Ni muda wa Mr Moss kutake over.” Mwaka 2001 alibadili jina kutoka Lil Bow Wow na kuitwa Bow Wow na sasa ni zamu ya Mr Moss
On 3:38 AM by Unknown in ,    No comments
Kundi la Mapacha jana (June 23) wametambulisha ngoma yao mpya baada ya ukimya wao wa muda mrefu, wimbo ambao wamedai wamemshirikisha muigizaji wa Bongo Movie Elizabeth Michael aka Lulu. Lakini Lulu leo amekana kushirikishwa katika wimbo huo kwa kusema kuwa hana taarifa zozote wala haujui wimbo huo.

Hiki ndicho alichokiandika Instagram:

“Mwe mwe mwe…!Mbona mnaninyasanyasa…’in Senga’s voice’
I swear sina idea na Huku kushirikishwa….au kuna Elizabeth Michael’Lulu’ mwingine!????
Dah…hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn”.
Wimbo mpya wa Mapacha unaoitwa ‘Time For The Money’ umetengenezwa na Tudd Thomas.