Tuesday, June 24, 2014

On 2:01 PM by Unknown in    No comments
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis Suarez alimng’ata Giorgio Chiellini. Godin alifunga bao hilo dakika ya 81 na kipa Buffon wa Italia alilazimika kuingia uwanjani dakika ya mwisho kusaidia nguvu ya kusaka bao, Azzuri ikihtaji sare tu kusonga mbele. Italia ilimpoteza mchezaji wake Marchisio aliyetolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Arevalo Rios dakika ya 60.
Mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo (kushoto) akibadilishana jezi na Edisnon Cavani wa Uruguay baada ya mechi

0 comments:

Post a Comment