Tuesday, July 1, 2014
On 4:08 AM by Unknown No comments
Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Asha Juma(24), ameuawa kwa kuchomwa kisu na mfanyakazi wake wa ndani.
Tukio hilo limetokea jana saa 4:00 asubuhi eneo la Sabasaba katika kata ya Utemini mjini Singida.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema mauti yalimfika karani huyo mara baada ya kuchomwa kisu sehemu ya titi la kulia na mfanyakazi huyo wa ndani aitwaye Valetina Kerenge(17).
Msichana huyo ambaye ni mwenyeji wa mkoani Mwanza wilayani Ukerewe, inasadikiwa alilifanya tukio hilo wakiwa ndani na baada ya hapo alipata kiwewe na kukimbilia nje ya nyumba aliyokuwa akikaa na kwenda kwa majirani kuomba msaada.
Inasemekana wakati juhudi za majirani za kunusuru uhai wake zikifanyika ili kumuwahisha hospitali kwa matibabu, ghafla marehemu huyo alianguka chini na kufariki papo hapo.
“Imesikitisha maana chanzo halisi hakijajulikana, maana msichana huyu alipoona mambo siyo alikimbia,” alisema Kamanda Kamwela.
Kamanda alisema tayari msako mkali wa polisi ulifanikisha kumpata majira ya saa 8 mchana akiwa katika harakati za kutoroka maeneo ya uwanja wa ndege.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi, na baada ya kuchunguza ndugu wa marehemu watakabidhiwa kwa taratibu za kuusafirisha mwili huo kuelekea mkoani Shinyanga kwa mazishi.
Jeshi la polisi linamshikilia msichana huyo kwa ajili ya mahojiano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Miley Cyrus updated her Instagram with lots of photoshopped pictures. This time, Justin Bieber 's Calvin Kl...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Will Smith , who is gearing up for his new film " Focus " with Margot Robbie , opens up about his experience in 25 y...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
Channel O walitisha sana na maandalizi ya mwaka huu wa 2014 ambapo magari mbalimbali yalitumika kuwaleta mastaa mpaka kwenye stage...
-
Yemen imesema wapiganaji wa kundi la al-Qaeda wamewaua watu sita katika mapi...
-
The Rock says his mom, Ata Maivia-Johnson and his cousin were struck HEAD ON by a drunk driver this week ... and luckily, they su...
0 comments:
Post a Comment