Friday, August 8, 2014
On 1:18 AM by Unknown No comments
Kwa mara ya kwanza staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameibuka na kuuelezea upande wa pili wa maisha yake kuwa kabla hajawa mwanamuziki alikuwa mwizi balaa!
Akizungumza na mwandishi wetu ana kwa ana jijini Dar es Salaam juzi, staa huyo alikiri kupitia katika majanga kibao maishani mwake likiwemo la kulala katika vituo mbalimbali vya polisi vya jijini Dar kufuatia kufanya matukio ya uhalifu.
“Kwanza kabisa nilikuwa nalala Feri na watoto machokoraa. Nilikuwa naona ndiyo maisha japokuwa nilijua kuna maisha mengine mazuri zaidi lakini ningeyapate?
“Dah! Yaani kusema kweli nilipita kwenye majanga makubwa sana jamani! Anyway, kimsingi ukweli wa maisha yangu siwezi kuuficha maana nitakuwa najiongopea bure kwani ni kweli niliishi katika maisha ya matukio sana,” alisema Nay.
Akizidi kutiririka , Nay ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Mr Nay aliweka bayana kwamba kwa nyakati tofauti aliwahi kuiba vitu mbalimbali (hakupenda kuvitaja) kwa watu wa karibu yake akiwemo Prodyuza Paul Mathysse ‘P Funk’ na kwenye studio moja iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar.
“Enzi zangu nilikuwa balaa, Majani mwenyewe (P. Funk) nilishawahi kumliza, nakumbuka pia kuna jamaa zangu walikuwa na studio ya muziki pale Mwenge nao niliwapiga.
“Tena hawa jamaa wa studio nakumbuka walikuja kinitaiti nikiwa kwenye msiba, wakanitia pingu na kunipeleka kituo cha polisi lakini bahati nzuri marehemu John Mjema, alikuwa mshikaji wangu sana, akaja kunitoa,” alisema Nay.
John Mjema ‘Bomba la Mvua’ alikuwa mwanamuziki wa Kizazi Kipya, alifariki dunia Februari 10, 2008 kwa kujichoma kisu cha shingo nyumbani kwake Mtoni Kijichi jijini Dar.
Nay akaongeza: “Kulala polisi nadhani ni kama mara saba hivi na mara zote aliyekuwa akinitoa ni John Mjema. Yeye wakati ule alikuwa akifanya kazi kule maeneo ya Feri.”
Pamoja na matukio hayo ambayo Nay ameyafanya, alisema alishatubu na kumwomba Mungu amsamehe kwani anaamini ujana ndiyo ulikuwa ukimsumbua.
“Yaliyopita si ndwele, kwa sasa naganga yajayo maana muziki unanilipa na naendelea na harakati zangu kama kawaida, nilishasahau hayo matukio ya ajabuajabu,” alimaliza Nay.
Miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata msanii huyo kupitia muziki wa Bongo Fleva ni kujenga nyumba Kimara-Rombo jijini Dar na gari la kutembelea aina ya Nissan Murano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Arnold Schwarzenegger was born and raised in Austria. But The Expendables 3 star looked like a true American as he left Cafe Roma in Beverly...
-
baada ya BET kutoa fulsa kwa production companies nyingi kwa ajili ya kurusha reality show ya chris brown sasa cheki akivyo sema..
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis ...
-
Baada ya habari za ndege ya Malaysia airline hivi sasa ajali nyingine imetoka karibu kabisa na Tanzania ambapo ni nchini Uganda. Ndege hiy...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Karrueche Tran mrembo ambae ni mpenzi wa mwimbaji staa wa dunia Chris Brown alihusika kama mtangazaji na kuhoji watu mbalimbali wal...
0 comments:
Post a Comment