Monday, October 6, 2014
On 5:55 AM by Unknown No comments

Rapper Noorah aka Babastylez amesema kama isingekuwa neema za Mungu, leo hii asingekuwepo
duniani.Akiongea kwenye kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV hivi karibuni, Noorah alidai alikuwa na tatizo la kujikunja kwa utumbo lililodumu kwa miaka 20. Amesema wakati tumbo likimuuma alikuwa akidhani ni vidonda vya tumbo.
“Doctor amekuja kunifanyia operesheni, baada ya operesheni akamuita mama pembeni. Akamwambia ‘mama huyu mwanao ana Mungu sana’. Maana kitu alichokikuta huko tumboni, hakuna binadamu anaweza akawa hai kwa hali ile. Utumbo wangu mdogo ulikuwa umejikunyata wote. Akauliza ‘alikuwa anapataje choo huyo!’
Alisema operesheni hiyo ilidumu kwa masaa sita na ilifanyika kwenye hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam.
“Nimetoka dokta anasema utumbo wangu ulikuwa umekuwa mdogo kama wa mtoto mchanga kwahiyo ulikuwa unapitisha chakula kwa tabu sana. Kwahiyo kipindi hicho nilikuwa nakula vyakula vya kusaga tu, na vyenyewe sometimes vingine havipiti.”
Pamoja na kuwa amepona tatizo hilo, Noorah amesema ana tatizo jingine linalofanya awe anapata vitu kama vifafa (seizure) ambavyo vimesababisha na ajali aliyopata mwaka 2005 iliyomfanya apate tatizo kwenye ubongo. “Sasa hivi dokta ameshanipa treatment na ameniomba nije nipate mind rest,” alisema Noorah ambaye kwa sasa amerejea kwao Shinyanga kama sehemu ya maagizo ya wataalam.
Noorah aliwaasa wasanii na watu wengine kuwa na desturi ya kuchunguza afya zao mara kwa mara kubaini matatizo yanayowasumbua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Miley Cyrus updated her Instagram with lots of photoshopped pictures. This time, Justin Bieber 's Calvin Kl...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
Will Smith , who is gearing up for his new film " Focus " with Margot Robbie , opens up about his experience in 25 y...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
Mara nyingi birthday party za washkaji huwa zinasindikizwa na umwagiwaji wa maji kwa mhusika,sasa unaambiwa hii ya Shetta imekua kibok...
-
Channel O walitisha sana na maandalizi ya mwaka huu wa 2014 ambapo magari mbalimbali yalitumika kuwaleta mastaa mpaka kwenye stage...
-
Diamond Platnumz ameingia Dar es salaam usiku wa July 10 mashabiki wengi wakiongozwa na mama yake,dada yake pamoja na mpenzi wake Wema S...
0 comments:
Post a Comment