Monday, July 14, 2014

On 6:27 AM by Unknown   No comments
Samsung imesitisha uhusiano na kampuni hiyo
Kampuni ya bidhaa za elektroniki ya, Samsung imesema kuwa imepata ushahidi wa kuwatumikisha watoto kinyume na sheria katika moja ya kiwanda cha kusambaza bidhaa zake nchini China cha Dongguan Shinyang
.
Samsung imesema kuwa iliichunguza kampuni hiyo baada ya madai kutoka kwa shirika la kupambana dhidi ya utumkishaji wa watoto ya Marekani 'China Labor Watch' kuituhumu kwa kuwatumikisha watoto.
Awali kampuni hiyo ya korea kusini ilikana kwamba baadhi ya kampuni zinazosambaza bidhaa zake zinawaajiri wafanyakazi walio chini ya umri wa miaka 16,lakini uchunguzi uliofanywa na shirika hilo umeilazimu kampuni hiyo kukiri makosa yake.
Takriban watoto watano walio chini ya umri wa miaka 16 walikuwa wakitengeneza baadhi ya sehemu za simu za samsung ,kulingana na uchunguzi wa siri wa shirika hilo la haki za wafanyikazi,lililo na makao yake mjini New York.
Watoto hao ambao wamekuwa wakifanya kazi bila kandarasi wamekuwa wakilipwa thuluthi mbili za mshahara wa mtu mzima.
Wasambazaji wa bidhaa za Samsung wanashtumiwa kwa kuvunja sheria za kazi za uchina kupitia kuwaruhusu watoto wadogo kufanyakazi katika kemikali mbali na kupuuza sheria za uchina kuhusu kazi za mda wa ziada ambapo hufanya kazi kwa masaa 11 katika zamu ya masaa 10.
Hivi majuzi kampuni ya samsung ilitoa matokeo ya ukaguzi wake kuhusu wasambazaji wa bidhaa zake nchini Uchina ambayo hayakupata ushahidi wowote kuhusu ajira ya watoto.
kampuni hiyo imeahidi kukata uhusiano wake na kampuni za usambazaji wa bidhaa zake iwapo itathibitisha madai hayo mapya.

0 comments:

Post a Comment