Thursday, July 24, 2014

On 1:34 AM by Unknown   No comments
Jeshi
la Polisi linawahoji watu nane wakiwemo Madaktari wa chuo cha kitabibu
cha IMTU kwa madai ya kutupa mabaki ya masalia ya binadamu katika msitu
mdogo uliopo eneo la Mpiji kata ya Mbweni wilayani Kinondoni Dar es
salaam.



Kamanda
wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema
kulipatikana mifuko 85 iliyobeba mabaki ya masalia hayo ya binadamu.




‘Imeonekana mara ya mwisho viungo hivyo vilikua katika chuo cha
Udaktari cha IMTU kinachofundisha kwa vitendo pia, sasa tunachunguza na
wamekubali kuhojiwa, maswali yanayofata ni kwanini viungo hivyo vilikua
pale kwa wingi kiasi hicho? kwa nini vilikwenda kutupwa? ‘ – Kova



Screen Shot 2014-07-24 at 3.44.25 AMKwenye
hii ishu pia hospitali ya taifa Muhimbili inachunguzwa ambapo mkuu wa
kitengo cha uhusiano kwenye hospitali hii ya taifa Aminiel Aligaesha
amesema >> ‘Sisi ni miongoni
mwa wanaochunguzwa kwa sababu ni hospitali mojawapo katika jiji la Dar,
mabaki yale hayakutoka hospitali ya taifa Muhimbili’



‘Kuharibika
kwa tanuru letu la kuchoma taka za kitabibu kama hizo hakuna uhusiano
na mabaki ya binadamu yaliyookotwa Tegeta, ni kweli tanuru liliharibika
February 2014 na mwezi April tukapata spea lakini tatizo jingine
likatokea na kipuri kingine kikaagizwa na mpaka sasa mafundi wanaendelea
kuitengeneza’ – Aminiel.




Kwa taarifa zaidi unaweza kumtazama  hapa chini

0 comments:

Post a Comment