Wednesday, August 20, 2014

On 12:24 AM by Unknown   No comments

G-Unit wameungana na wasanii wengine kupaza sauti yao kwa kufanya wimbo kuonesha jinsi wanavyopinga mauaji ya kijana mweusi Michael Brown aliyekuwa na umri wa miaka 18, aliyeuawa kwa risasi kadhaa na afisa wa polisi ‘mzungu’ huko St. Louis, Missouri, August 9.
Kundi hilo limeachia wimbo unaoitwa ‘Aaah Sh*t’ ambao unalenga katika kuwaponda polisi wote waliowahi kufanya mauji ya raia walioonesha ishara ya kutii sheria kwa kunyoosha mikono miwili juu.
“Now why the f**k did you call them cops? / Throw your hands up, you still gettin’ shot / Here they come now, they out on patrol / They done killed a few, they finna kill some more.” Ni sehemu ya mashairi ya wimbo huo.
Wasanii wengi wa Marekani hasa weusi wamelaani vikali kitendo hicho cha kikatili na cha kibaguzi na wanadai hakuna taarifa zilizowahi kudai polisi mweusi amempiga risasi kijana wa kizungu. Ila ripoti za polisi wazungu kuwauwa vijana weusi zipo nyingi.
Ripoti ya uchunguzi binafsi iliyotolewa kwa vyombo vya habari na wakili wa familia ya Michael Brown, Madaktari na wawakilishi wa familia, inaonesha kuwa Michael Brown alipigwa risasi juu kidogo ya paji la uso ambayo ilijeruhi pia jicho lake.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa risasi nyingine ikimpata katika eneo la mkono ambalo kwa mujibu wa timu ya madaktari eneo hilo linaonesha wazi kuwa marehemu alikuwa amenyoosha mikono yote juu kuashiria kutii amri. Mwili wa kijana huyo umeonesha kuwa alipigwa risasi nyingi katika maeneo mbalimbali.

Makundi mbalimbali ya waandamanaji nchini Marekani yanayotumia kauli mbiu ya ‘Hands Up Don’t Shoot’ yameingia mitaani kwa amani huku wengine wakifanya uharibifu na kulazimu polisi kuwatawanya.

Cover la wimbo wa G-Unit wenye michoro ya ripoti ya jinsi Michael Brown alivyopigwa risasi
Usikilize hapa

0 comments:

Post a Comment