Thursday, July 3, 2014
On 2:21 PM by Unknown No comments
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameonesha kukerwa kwake na mastaa wa Bongo ambao ni Waislam na wanaishi na wenza wao bila ndoa, hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Akizungumza na mwandishi wetu juzi, Shehe Alhad alisema kwa mujibu wa imani ya Dini ya Kiislam, Muislam hupaswa kufunga mwezi mtukufu kama hana matatizo ya kiafya.
Alisema kwa wale Waislam ambao wapo katika uhusiano usio wa ndoa nao hutakiwa kujiandaa kwa mwezi huo wa toba kwa kutengana na wenza wao mpaka mfungo utakapomalizika.
Shehe huyo aliongeza kuwa ni makosa kwa Muislam kufunga akiwa anaishi na mpenzi wake pasipo ndoa na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo ni sawa na kushinda na njaa.
“Mwislam yeyote asiye katika ndoa lakini akafunga mwezi mtukufu hali akiwa anaishi na mpenzi wake ni bure na suala hilo ni sawa na kujikalisha na njaa tu. Hata kama hawatashiriki zinaa lakini tunaambiwa tusiikaribie zinaa.
“Hivyo lazima atengane na mpenzi wake huyo kwa kukaa naye mbali na kusiwe na mawasiliano ya kimapenzi kati yao,” alisema Alhad.
Wakali katika tasnia ya filamu Bongo Wema Sepetu na Snura Mushi.
Kwa kusema hivyo, Shehe Alhad aliwagusa mastaa wa Bongo ambao wanajulikana kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini hufunga kila ufikapo Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Baadhi ya mastaa wasio kwenye ndoa lakini wamefunga mwezi huu walizungumza na waandishi wetu ambapo walidai kutimiza masharti ya mwezi huo kwa kutengana na wenzi wao, baadhi yao ni:-
Snura Mushi ambaye yupo katika uhusiano wa kimapenzi na Dj Hunter wa Maisha Club mkoani Mbeya, amesema:
“Mwenzangu yupo Mbeya hivyo tumetengana. Nilijiandaa miezi miwili kabla kwa ajili ya kufunga mwezi huu. Huwa tunawasiliana tu kwa salamu na mambo ya kawaida.
”
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo Rose Ndauka.
Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ambaye pia yupo katika uhusiano na dogo Mbongo Fleva, Nuhu Mziwanda naye amefunguka: “Naipenda sana dini yangu ndiyo maana nimetengana na mwenzangu kwa sasa. Tunazungumza jioni tena baada ya kufuturu.”
Rose Ndauka, yeye yupo kwenye uhusiano na mzazi mwenziye, Malick Bandawe:
“Yah mimi mwenyewe nimefunga na mwenzangu naye amefunga, tumetengana mimi nimerudi kwa mama mpaka mwezi uishe. Huwa tunapigiana simu kwa ajili ya kunijulia hali yangu na ya mtoto.”
Wema Sepetu hakupatikana kwenye simu, lakini na yeye yupo kwenye uhusiano na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wote wakiwa kwenye imani inayowataka kufunga mwezi huu kama hawana matatizo ya kiafya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Nicki Minaj didn't seem to have big problems with hilarious memes appearing on the internet following the release of her...
-
Miley Cyrus updated her Instagram with lots of photoshopped pictures. This time, Justin Bieber 's Calvin Kl...
-
Mr Blue aka Kabayser ameanzisha taasisi ya ‘Micharazo Foundation’ itakayoanza kupokea wasanii wapya na pia itakuwa sehemu ya kukuza vipaj...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
Mara nyingi birthday party za washkaji huwa zinasindikizwa na umwagiwaji wa maji kwa mhusika,sasa unaambiwa hii ya Shetta imekua kibok...
-
Amber Rose was a guest on the Breakfast Club last week , and she threw some shade towards Tyga and Kylie Jenner, alluding that the two wer...
-
Yemen imesema wapiganaji wa kundi la al-Qaeda wamewaua watu sita katika mapi...
-
The Rock says his mom, Ata Maivia-Johnson and his cousin were struck HEAD ON by a drunk driver this week ... and luckily, they su...



0 comments:
Post a Comment