Wednesday, August 6, 2014
On 5:20 AM by Unknown No comments
Ile kesi ambayo inahusu Kampuni ya Apple na Samsung kwa sasa zimekubaliana kuachana na kutupilia mbali kesi zote zilizofunguliwa Marekani zikiwa zimeshitakiana,Kampuni hizo zilizozana kuhusu uanzilishi wa vifaa vya kielektroniki katika nchi kadhaa ikiwemo Uingereza, Korea ya kusini,Japan na Ujerimani.
Kampuni zote mbili zilikuwa zimewasilisha mashitaka mahakamani lakini katika taarifa yao ya makubaliano ya hivi karibuni,kampuni zote mbili zimesema mzozo huo haukua na jambo lolote linalohusiana na leseni na hivyo basi zitaondoa kesi hizo Marekani.
Mwafaka huu kati ya kampuni hizo mbili umeafikiwa baada ya miaka kadhaa ya migogoro ambapo Migogoro yao ilianza mwaka 2011 baada ya Apple kuishtaki Samsung huko Marekani na kudai kuwa kampuni ya Galaxy iliyoko Kusini mwa Korea ilitumia miundo ya iPhone na iPad.
Kampuni ya Galaxy ilijibu mashtaka ya Apple na kuishtaki kwa misingi ya kuingilia haki zake za uanzilishi wa programu za picha,muziki, na picha za video, na pia jinsi ya kunasa na kutuma picha za video mtandaoni.
Apple pia iliwasilisha mashtaka ya kupinga madai ya uanzilishi na Galaxy lakini hatimaye kuafikiana kutupilia mbali kesi hizo za uanzilishi,Apple ilishinda kesi mbili dhidi ya Samsung miaka michache iliyopita.
Mwezi Mei, mahakama moja ya Marekani iliamuru Samsung kulipa dola million 119.6 kwa Apple kwa kuingilia haki zake za uanzilishi. Apple ilikuwa imewasilisha ombi kulipwa dola milioni 2.2.
Vile vile, mahakama hiyo ilikataa kauli kuwa Apple iliingilia haki Fulani za Uanzilishi wa Samsung na kulipa Samsung dola 158,000.
Hata hivyo Samsung ilikana mashtaka hayo na kutaka kulipwa dola milioni 6 kwa madai kuwa Apple ilingilia haki zake za Uanzilishi wa simu Fulani za kisasa zinazoweza kunasa na kupeperusha picha za video
Miaka miwili iliyopita, baraza lingine la waamuzi liliamuru Samsung kulipa Apple dola bilioni 1.05 kwa kutumia maarifa ya Apple kutengeneza vifaa vyao, kinyume na sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Arnold Schwarzenegger was born and raised in Austria. But The Expendables 3 star looked like a true American as he left Cafe Roma in Beverly...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis ...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Baada ya habari za ndege ya Malaysia airline hivi sasa ajali nyingine imetoka karibu kabisa na Tanzania ambapo ni nchini Uganda. Ndege hiy...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
Kuna watu wengi maarufu ambao pesa zao nyingi hupeleka kwenye bata na mambo mengine, lakini kiungo wa timu ya taifa ya Ghana sulley Muntari...
0 comments:
Post a Comment