Thursday, September 11, 2014

On 4:35 AM by Unknown   No comments

Leo dunia inakumbuka tukio kubwa na baya la kigaidi lilolofanywa na kundi la Al Qaeda chini ya uongozi wa Osama Bin Laden mwaka 2001 baada ya kushambulia majengo ya kitengo cha ulinzi cha Marekani jijini Washington na jengo la biashara huko New York na kuuawa takribani watu 3,000.
Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kufuatia vitendo vya kigaidi vinavyozidi kushamiri katika ukanda wa Afrika hususani kundi la Alshabaab linalofanya mashambulizi ya kushitukiza katika nchi jirani ya Kenya.
Hayo yamesemwa na mnadhimu wa kikosi cha usalama barabarani (SACP), Johansen Kahatano katika kipindi cha Sunrise cha 100.5 Times Fm.
Kahatano ameeleza kuwa hivi sasa kundi la Alshabaab lipo katika harakati ya kulipiza kisasi kufuatia kuuawa kwa kiongozi wao na majeshi ya Marekani hivyo raia wanapaswa kuwa makini na kutoa taarifa mara moja polisi pale wanapomtilia mashaka mtu yeyote.
“Nitoe wito tu kwa wananchi kwamba tuchukue tahadhari ya kutosha sisi wenyewe kwa maana ya kutaka kujilinda dhidi ya jamii inayotuzunguka. Unapokuwa na mashaka na mtu ambaye hafahamiki sawasawa, awe amebeka kitu ambacho kinatia shaka. Hasa kwenye mabasi pale unamuona mtu anasafiri na mzigo wake halafu anashuka anauacha pale kwenye basi. Hata katika mikusanyiko ya watu wengi, ukishakuwa na mashaka na mtu lazima taarifa itolewe kwa askari.” Ameeleza.
Kuhusu September 11, 2011:
Ilikuwa siku ya Jumanne, September 11 mwaka 2001 ambapo kundi la kigaidi la Al Qaeda chini ya uongozi wa Osama bin Laden liliteka ndege za Marekani, American Airlines Flight 11 na United Airlines Flight 175 na kuzigongesha kwenye matawi ya Kusini na Kaskazini ya jengo la ulinzi la Pentagon, Washington na Jengo la Biashra ‘World Trade Center Complex’ huko New York.
Ndege nyingine zilizotekwa haziweza kutekeleza shambulizi na kulipuka wakati abiria walipokuwa wanafanya jitihada za kujiokoa mikononi mwa watekaji.
Watu takribani 3,000 walipoteza maisha na kusababisha hasara ya zaidi ya takribani $ billion 10.
Osama Bin Laden alithibisha kuwa kundi hilo ndilo lililotekeleza tukio hilo japo alikanusha kuhusika na tukio la shambulizi la balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2004.
Osama alitaja sababu za kutekeleza tukio hilo kuwa ni uwepo wa vikosi vya Marekani nchini Saudi Arabia na vikwazo ilivyowekewa nchi ya Iraq na sapoti ya Marekani kwa Israel katika vita ya ukanda wa Gaza.
Shambulio la September 11 lilikuwa shambulio baya la kigaidi katika historia ya Marekani ambapo maafisa wengi zaidi na raia walipoteza maisha.
Marekani ilianzisha mashambulizi makali nchini Afghanistan wakimsaka Osama Bin Laden na vikundi vya Taliban vilivyokuwa vimemficha.
Vikosi vya Marekani vilimuua Osama bin Laden mwaka 2011 nchini Pakstani baada ya msako wa miaka 10.

0 comments:

Post a Comment