Thursday, June 26, 2014
Mwanamuziki Diamond amefunguka kuhusu madai ya baadhi ya wasanii kuwa aliwaibia idea au nyimbo zao na kuzifanya zake.
Ameeleza kuwa malalamiko yao hayana ukweli kwa kuwa kuna maneno ya ambayo yamezoeleka na yanaweza kutumiwa na watu wote lakini anapoyatumia hutokea msanii aliyetumia maneno kama yale na kudai kuwa ameiba idea yake.
Ametoa mfano wa nyimbo kama Moyo Wangu ambayo anasema baada ya kuimba wasanii wengine waliimba pia lakini hakuwahi kujitokeza kusema ameibiwa kwa sababu neno hilo linaweza kutumika na kila mtu kwa ufundi wake.
Diamond ameeleza pia kuhusu tuhuma za Wababa (ingawa hakumtaja jina) kuwa alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na sasa anauita Mdogomdogo.
“Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi…mimi nimezaliwa Tandale nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo, Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani hii ni nyimbo.
“Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyo ile nyimbo ya mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswali hayo kabisa.”
Kwa hisani: Timesfm.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Arnold Schwarzenegger was born and raised in Austria. But The Expendables 3 star looked like a true American as he left Cafe Roma in Beverly...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis ...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Baada ya habari za ndege ya Malaysia airline hivi sasa ajali nyingine imetoka karibu kabisa na Tanzania ambapo ni nchini Uganda. Ndege hiy...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
Kuna watu wengi maarufu ambao pesa zao nyingi hupeleka kwenye bata na mambo mengine, lakini kiungo wa timu ya taifa ya Ghana sulley Muntari...
0 comments:
Post a Comment