Tuesday, August 19, 2014
On 1:05 AM by Unknown No comments
Mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali Kiba amefunguka kuhusu mambo yaliyomkwaza kutoka kwa Diamond miaka michache iliyopita baada ya mkali huyo kutoka na wimbo wa ‘Kamwambie’ uliogeuka kuwa wimbo wa taifa wa Bongo Flava kwa muda.
Akiongea na kipindi cha Mkasi, Ali Kiba ameeleza kuwa yeye ndiye mtu aliyepitisha ombi la Diamond kurekodi katika studio za SharoBaro kwa kuwa wakati huo alikuwa mdau mkubwa katika uongozi wa studio hizo lakini matokeo yake yalimgeukia hadi kuamua kujitoa katika team hiyo.
Ameeleza kuwa mara baada ya Diamond kutoka na Kamwambie, aliona gazeti moja lililokuwa lililomkariri akisema kuwa yeye ndiye ‘fimbo’ ya Alikiba na amekuja kumfunika.
Hata hivyo maneno yaliyowekwa kaitika gazeti hilo yalianza kuaminika kwa Ali Kiba baada ya kukutana nae mara kadhaa kwenye shows.
“Lakini nilishawahi kukaa na Diamond katika mikutano ya Shows ambazo tunaitwa pamoja wasanii na nini na nini. Mimi napendaga kuongea nae kama mdogo wangu kwa sababu the way nilivyokuwa nikimtreat ni kama wadogo zangu wengine akina Bob Junior akina nani… Nilimsikia akiongea sana kwamba nimekufunika kwenye show fulani, nimekufunika kwenye show fulani. Kwa kweli the way nilivyokuwa nikimtreat kama mdogo wangu. Kwa hiyo yeye alikuwa ameconcentrate sana katika kunifunika.” Alieleza Ali Kiba.
“Mimi sio mtu wa kumind sawa. Kwa hiyo alivyokuwa anaongea anajifurahisha. Hata kama amenifunika mimi nilikuwa naweza kumpigia makofi vilevile. Si nataka afanikiwe. Kwanza nafurahi. Napenda sana challenge. Inakufanya unaaamke.” Aliongeza.
Kujirudia kwa neno ‘kufunika’ kila walipokuwa akikaa na Diamond kuligeuka kuwa kero kwa Ali Kiba huku mengine yakipenya kutoka kwa watu wake wa karibu.
“Kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa kinahappen tukiwa karibu hivi, ni hivyo vitu ambavyo akizungumziwa nimekufunikaa..nimekufunika. Nikawa nikitoa video nasikia maneno, kwamba ‘Ali amesikia maneno nimetoa hii na yeye ametoa hii’. Mi sijawahi kumsikia mwenyewe akisema. Ila watu wake wa karibu wa karibu wanakuja wanasema. Unaweza kumjua mtu tabia yake kwa kumuangalia, kwa kuishi nae.”
Ali ameeleza kuwa hata baada ya kuamua kukaa kimya amlee mwanae wa kiume alisikia tena maneno kutoka kwa mwimbaji kwa Diamond kuwa amemkimbia.
Hata hivyo, hii ilikuwa story ya zamani ambayo wengi wanaweza kuwa nayo lakini ikamhusu mtu ambaye kwa sasa amekuwa rafiki wa kudumu.
Hivi karibuni Ali Kiba alisema kuwa hana tatizo lolote na Diamond na kuwataka watu wasimgombanishe na msanii huyo.
Ni muda wa biashara. Yaliyopita si ndwele (maradhi) tugange yajayo kwa maendeleo ya Bongo Flava. Kilichobaki ni ushindani wa kibiashara kama alivyosema Babu Tale
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Nicki Minaj didn't seem to have big problems with hilarious memes appearing on the internet following the release of her...
-
Miley Cyrus updated her Instagram with lots of photoshopped pictures. This time, Justin Bieber 's Calvin Kl...
-
Mr Blue aka Kabayser ameanzisha taasisi ya ‘Micharazo Foundation’ itakayoanza kupokea wasanii wapya na pia itakuwa sehemu ya kukuza vipaj...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
Mara nyingi birthday party za washkaji huwa zinasindikizwa na umwagiwaji wa maji kwa mhusika,sasa unaambiwa hii ya Shetta imekua kibok...
-
Amber Rose was a guest on the Breakfast Club last week , and she threw some shade towards Tyga and Kylie Jenner, alluding that the two wer...
-
Yemen imesema wapiganaji wa kundi la al-Qaeda wamewaua watu sita katika mapi...
-
The Rock says his mom, Ata Maivia-Johnson and his cousin were struck HEAD ON by a drunk driver this week ... and luckily, they su...
0 comments:
Post a Comment