Friday, June 27, 2014
On 6:09 AM by Unknown No comments

Anaitwa Amina Maige au Amina kumeza
Mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige (42) jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kujibu shtaka la kumjeruhi kwa meno mfanyakazi wake wa ndani Yusta Lucas.Amina akiwa amevalia vazi la baibui na kujifunika usoni kwa nikabu hali iliyosababisha kutoonekana sura kabla ya kuamriwa na Mwendesha Mashtaka ajifunue, alifikishwa mbele ya Hakimu Yohana Yengola ambapo alikana shitaka linalomkabili.

Yusta dada wa kazi alokuwa akiteswa na boss wake kwa muda wa miaka mitatu. Boss mwenyewe ndio huyo bidada hapo juu wala hafananii na unyama alokuwa akiufanya kwa mtoto wa watu.


Wakili wa Serikali, Tumaini Mfikwa akisoma hati ya mashtaka alidai katika kipindi cha kati ya 2012 na 2014 katika eneo la Mwananyamala kwa Manjunju, Amina huku akijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria, alimjeruhi Yusta kwa kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia majereha makubwa.

Yupo segerea hivi sasa na na jana kesi yake ilisomwa.
Mfikwa alidai upelelezi umekamilka na aliomba tarehe ya kusikilizwa pamoja na mahakama kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa kwa kuwa hali ya usalama wake ni tete.
Hakimu Yongolo alikubaliana na ombi hilo na mtuhumiwa alirudishwa rumande hadi Julai 10, mwaka huu, kesi yake itakapoanza kusikilizwa.
Amina ambaye ni mtaalamu wa kompyuta katika kampuni ya Ocean Air Flight, aliiomba mahakama impe dhamana akapate matibabu kwa kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo, wakili Mfikwa aliiambia Mahakama kuwa mtuhumiwa atapatiwa matibabu akiwa rumande.
Juni 12, mwaka huu wakati Amina anafikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, shughuli katika mahakama hiyo zilisimama kwa takribani saa mbili baada ya watu waliokusanyika ndani na nje kutaka kumuona na kuanza kuzomea na kupiga kelele za kumtaka ajifunue uso.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Brad Pitt has owned a gun since he was very young. In a new interview with Radio Times to promote his new flick " Fury ", the a...
-
Channel O walitisha sana na maandalizi ya mwaka huu wa 2014 ambapo magari mbalimbali yalitumika kuwaleta mastaa mpaka kwenye stage...
-
Miley Cyrus updated her Instagram with lots of photoshopped pictures. This time, Justin Bieber 's Calvin Kl...
-
Sio Wakati Wote Ni Wa Kazi Hata Kmaa Ni Mtu Maarufu Kuna Muda Unatakiwa Kukutana Na Watu Tofauti Na Kujipa Raha kwa Nafasi Kama Unavyomuo...
-
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Asha (31) ambaye ni mke wa mtu, amejikuta akiachika katika ndoa yake baada ya kudaiwa kumuun...
-
Justin Bieber ambaye hivi sasa yuko katika kipindi cha matazamio ameripotiwa kuhatarisha maisha ya watembea kwa miguu katika eneo la Beve...
-
Yemen imesema wapiganaji wa kundi la al-Qaeda wamewaua watu sita katika mapi...
0 comments:
Post a Comment