Thursday, September 11, 2014
On 1:24 AM by Unknown No comments
Mahakama nchini Mexico imewafunga jela miaka 30 kila mmoja ndugu wa familia moja kwa kosa la kushirikiana kumtoa macho kwa kutumia kijiko mtoto wao mwenye umri wa miaka mitano baada ya kukataa kumuabudu shetani.
Mtoto huyo aliyetajwa kwa jina la Fernando Caleb Alavarado Rios aliamrishwa kufumba macho mbele ya mama yake mzazi, mama yake mdogo, babu yake na wajomba zake wakati ambapo walikuwa wanamuomba shetani ajitokeze ili awasaidie kuepukana na janga la tetemeko la ardhi!
Lakini kijana huyo alikuwa anaogopa kwa jinsi utaratibu wa ibada hiyo ya kishetani iliyovyokuwa inaendeshwa hivyo akakataa kabisa kufanya hivyo.
Katika hali isiyo ya kawaida, mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Maria del Carmen Garcia Rios alimkamata kwa nguvu na kuwataka wenzake wamsaidie kumtoa macho. Mama yake mdogo alishirikiana na mama yake na wakatekeleza kitendo hicho cha kinyama.
Mama yake Fernando
Kwa mujibu wa UK Daily Mail watu hao walikamatwa baada ya jirani yao kusikia makelele na kujaribu kufanya uchunguzi kujua kinachoendelea.
“Tuliweza kusikia makele na tulikuwa tunapiga hodi kwa nguvu kwenye mlango wao lakini hakuna mtu aliyetujibu, baadae polisi wa patrol alikuwa anapita na wanawake waliokuwa na sisi walikimbia barabarani na kumuita, walikuja polisi wengi na walitumia nguvu kuingia ndani.” Alieleza jirani huyo aitwae Joaquin Arguello.
Polisi aliyejitambulisha mahakamani hapo kwa jina la Benet Curiet aliyefika kwenye eneo la tukio alieleza kuwa baada ya kufika pale alikuta damu zikiwa zimetapaka, aliwahoji watu hao na mama yake alijitambulisha vizuri na kukiri kuwa yeye na mdogo wake ndio waliosaidiana kumtoa macho mtoto huyo baada ya kukataa maagizo yao wakati wa ibada ya shetani.
Jana (September 10) ilikuwa ni miaka miwili tangu lilipotokea tukio hilo May 2012, na mahakama imewahukumu wote waliokuwa katika ibada hiyo kifungo cha miaka 30 jela.
Mtoto Fernando hivi sasa hana uwezo wa kuona na madaktari wamempa miwani maalum na yuko katika uangalizi wa serikali.
Chanzo: UK Daily Mail
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Slider
MusicView All
TechnologyView All
PicturesView All
GamesView All
Labels
Category
Ads
Text
Find Us On Facebook
Link List
Contact Form
Blogroll
Flickr Images
728x90 AdSpace
Label
FashionView All
Latest News
Popular Posts
-
It's good to be Iron Man — Robert Downey Jr. once again leads Fo...
-
Tumezoea kusikia wakati wa kufunga ndoa watu wakila kiapo kuwa watapendana hadi kifo kitakapowakuta, kia...
-
Arnold Schwarzenegger was born and raised in Austria. But The Expendables 3 star looked like a true American as he left Cafe Roma in Beverly...
-
baada ya BET kutoa fulsa kwa production companies nyingi kwa ajili ya kurusha reality show ya chris brown sasa cheki akivyo sema..
-
Lil Wayne ni msanii wa Hiphop lakini aliwahi kujaribu kutoa album ya rock ambayo inaitwa Rebirth yenye hit singles kama Knock Out na Porm ...
-
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis ...
-
Baada ya habari za ndege ya Malaysia airline hivi sasa ajali nyingine imetoka karibu kabisa na Tanzania ambapo ni nchini Uganda. Ndege hiy...
-
Brad Pitt and Angelina Jolie will finally tie the knot, only for a movie. According to a scoop from The Hollywoo...
-
Karrueche Tran mrembo ambae ni mpenzi wa mwimbaji staa wa dunia Chris Brown alihusika kama mtangazaji na kuhoji watu mbalimbali wal...
0 comments:
Post a Comment